RAMADHANI MWEZI WA MAVUNO KWA WAISLAMU
Waislamu wote Duniani wameingia mwezi
mtukufu wa Ramadhani mwezi mosi, mwezi huu ni mwezi wa toba hususani kwa
waumimi wa dini hiyo. Kila kitu kina sheria na taratibu zake.

MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI
Mwezi huu unasheria zake ingawa binadamu
anatakiwa akae na kuishi katika misingi na utaratibu ambayo Mwenyezi
Mungu ameupanga na kuufundisha kwa mitume yake mbalimbali aliyoileta kwa
ajili ya kufikisha ujumbe juu ya ukubwa wake.
Mwezi huu unafadhila kubwa kwa Imani ya
Dini ya Kiislam una fadhila ambayo kila aliyekuwa katika imani hiyo
anatamani afike ndani ya mwezi huo wenye mafungu 3, yaani kumi la
kwanza, kumi la pili, kumi la tatu na la mwisho, nyuma ya ramadan kuna
swala ya sunna ya taraweeh ambayo imeambatana na fadhila kadha wa kadha
tutaziangazia siku za usoni
VITU GANI INATAKIWA UFUNGE?
Funga hulipwa moja kwa moja na Mungu kwa
imani ya kiislam, lakini katika kufunga inatakiwa ufunge vyote. Waislam
wengi hudhania Kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani ni kufunga kula peke
yake, kumbe sio tu kula na kunywa bali kuna vingine inatakiwa ufunge
viende sambamba.
1.ULIMI
uache kuongea maneno yasiyofaa mfano kusengenya,kutukana na hata koropoka.
2.KUANGALIA VISIVYO FAA
Macho moja ya vitu vinavyoharibu saumu
za watu uyachunge macho yako ili uhifadhike kwa kuangalia vitu ambavyo
havita kuingiza kwenye matamanio au kumua Mwenyezi Mungu.
3.KULA NA KUNYWA
Pia hili la kula na kunywa haitakiwi ule
hadi muda ambao umepangwa kutokana na mabadiliko ya muda haswa kuanzia
saa kumi na mbili na nusu jioni kuacha halikadhalika kuacha yote yaliyo
katazwa.
No comments:
Post a Comment
Comment here